- Kumwambia kila mtu ndoto yako: kwa upande mmoja ni sahihi kabisa kumwambia mtu ndoto zako ambaye unadhani ataweza kukusaidia kufikia hiyo ndoto yako na siyo kumwambia kila mtu ndoto zako kwani wengine watakukatisha tamaa. Mfano unataka kufanya jambo fulani kwa siku za hapo baadae alafu unamshirikisha ndoto zako mtu ambaye huwa ana mawazo/mtazamo hasi au tofauti kwa hicho ulichomweleza,
- Kurithika: adui mkubwa wa mafaniko yako ya sasa ni mafanikio yako ya zamani. Watu wengi wamekuwa wakijikuta hawafikii zile ndoto zao kwa sababu ya mafaniki madogo waliyoyapata wakati wakiwa njiani kufikia zile ndoto zao. Kiabaya zaidi kwenye kurithika ni kwamba inafanya mtu siyo tu kushindwa kufikia ndoto zake bali pia kusahau ndoto zake. Mfano kwa mcheza soka ana ndotoza kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania lakini akishafika simba au Yanga anaridhika na kuhisi amefikia mafanikio makubwa sana. Tumia mfano huu uweke kwenye maisha yako ya kawaida.
- kushindwa mara kwa mara: hapa kuna na mtihani mkubwa kwa watu wengi kuvuka kwani imeshakuwa desturi watu kuangali kitu kilicho washinda watu wengine na kuona kama na wenyewe kita washinda. Mfano utasika mtu anasema "kitu fulani kilimshinda mtu fulani, mimi ndiye nitakaye kiweza?" ukiangalia maneno kama hayo yanaonesha kuwa watu wengi wanaangalia watu walioshindwa kwa kufanya kitu fulani lakini wanasahau kuwaangalia watu waliofnikiwa kwa kufanya kitu cha aina hiyo hiyo moja.
- kokosa ujasiri/udhubutu/kujiamini; hivi ni vitu tofauti ila kwa hapa vinaweza vikawa vinaleta matokeo ambaye yanaweza kuwa yanafanana. kuto kujiamini husababishwa na tabia kwani kwa zaidi ya 80% ya vitu tunavyofanya vinatokana na tabia. Kwa hiyo mtu akiwa hajiamini/adhubutu/ajaribu vya kutosha inakuwa ni vigumu kwa yeye kufikia ndoto zake. Mfano mtu anataka kuanzisha biashara ila anaogopa kufungua/kufanya hiyo biashara kwa hofu tu atapata hasara
Sunday, June 4, 2017
VITU GANI VINAVYOFANYA NDOTO ZA MTU ZISIFANIKIWE
Kuna vitu vingi vinavyofanya mtu asifikie kile alichokuwa anategemea kukifanya kwa siku za usoni. Hizi ni baadhi ya sababu za kwa nini ndoto hazifnikiwi
Wednesday, May 31, 2017
TANDIKA MIKEKA: LVERPOOL YATHIBITISHA KUMNYAKA DOMINIC SOLANKE
TANDIKA MIKEKA: LVERPOOL YATHIBITISHA KUMNYAKA DOMINIC SOLANKE: . Liverpool imefikia makubaliano na Dominic Solanke. mshambuliaji huyo anatarajiwa kujiunga na Liverpool baada ya mkaba wake na Chelsea kui... soma zaidi
Tuesday, May 30, 2017
ANGELA KAIRUKI: HAKUNA AJIRA ZA WALIMU WA SANAA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, (Angela Kairuki) amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari
Angela
Kairuki amesema hayo leo bungeni na kusisitiza kwamba kila shule
itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao
"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki
Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema
serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika
mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa
serikalini.
"Katika mwaka wa fedha
2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa
kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa
fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta
mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila
sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma" -alisema Kairuki
Angela Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, (Angela Kairuki) amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari
Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kusisitiza kwamba kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao
"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki
Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema
serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika
mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa
serikalini.
"Katika mwaka wa fedha
2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa
kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa
fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta
mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila
sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma" -alisema Kairuki
TANDIKA MIKEKA: LIVERPOOL, CHELSEA NA MAN CITY ZAPANIA KUBOMOA KIK...
TANDIKA MIKEKA: LIVERPOOL, CHELSEA NA MAN CITY ZAPANIA KUBOMOA KIK...: Liverpool ni moja ya vilabu vya EPL ambavyo vimejianda kuharibu kikosi cha Monaco kwa kuwawinda baadhi ya nyota wake katika majira ya joto....

Wednesday, April 19, 2017
MABADILIKO YANAYO KUATHIRI WEWE MWAJIRIWA NA AJIRA YAKO 👇🏽
✍🏽Kwa Tanzania sasa hivi kupoteza kazi yako ni rahisi sana. Unaweza kwenda kazini leo ukakuta umefukuzwa.⌚
Teknolojia inabadilisha kila kitu. Baada ya muda mfupi unaweza kukuta kazi yako inafanywa na mashine.
Huna uhakika na kampuni unayofanya nayo kama itabaki miaka 20 mbele inaweza pia ikafa.
Kumbuka Sikwambii haya kukutia hofu ni Ukweli ili ujiandae Lolote laweza kutokea.
Mambo uliyokua huyajui:-
• Hakuna Tajiri alieajiriwa, matajiri wote wanamiliki biashara zao wenyewe. Usifikiri kuwa tajiri kwa kupitia kwenye ajira.
• Huwezi kua tajiri kwa kutegemea mshahara wako anza sasa kufikiria na kufanya, buni mfumo utakaokutengenezea kipato wakati upo kwenye ajira kipato hicho kikizidi mshahara na fanya mpango uache kazi.
• Kama hujui ni kwamba boss wako hana mpango wa kubadili maisha yako furaha yake yeye ni aone unamfanyia kazi kwa bidii. Ukiumwa leo ukabaki nyumbani miezi mitatu ukirudi kazini utakuta nafasi yako imeshachukuliwa.
• Haijalishi una elimu kubwa kiasi gani au ndogo kiasi gani mwajiriwa ni mwajiriwa tu wote wana hatari moja/wote wanamfanyia kazi mtu, ukifukuzwa kazi leo maisha yako lazima yatayumba.
• Kilio kimoja cha kila mwajiriwa ni mishahara haikutani kamwe. Unaweza kubadili hali hiyo leo kwa kua na mfumo wako unakutengenezea pesa nje ya ajira.
• Usipoteze muda kuomba uongezewe mshahara au upande cheo waza kumiliki biashara yako mwenyewe.
• Mshahara ukiongezeka ujue utatakiwa ufanye kazi nyingi zaidi/uzalishe Zaidi, ukipanda cheo ujue na majukumu yatakua mengi Zaidi. Pesa utakayoongezewa huwezi kuifurahia tena.
• Kwenye mfumo wako mwenyewe ni kwamba kuna wakati utakua haupo lakini pesa zinaendelea kutengenezwa.
• Kama unafarijiwa na mafao utakayopata uzeeni piga mahesabu ni kiasi gani utapokea na uone jinsi gani unapoteza muda.
• Mafao unayoyasubiria baada ya miaka 40 ya ajira ungeweze kutengeneza mara 50 yake na kwa muendelezo yaani hiyo miaka 40 ya ajira ni miaka 5 tu inaweza kukufanya wewe uanze kuishi maisha ya kipato kinacholingana na mafao yako.
• Ajira yako haikulindi bali inakufanya uwe mtumwa unauza muda na nguvu zako kila siku kipato ambacho siku zote hakitakaa kikutoshe.
• Sikwambii haya ili uache kazi leo lah! Anza kujitengenezea mfumo leo ili undoke hapo bila maumivu wala hofu yeyote.
• Zipo biashara nyingi za kuanza ukiwa kwenye ajira lakini changamoto kubwa ni kwamba zitakukosa wewe kwasababu upo kwenye ajira hivyo ukuaji wake utakua kwenye hatari kubwa sana.
• Lakini zipo biashara ambazo unaweza kutenga ule muda wako wa ziada baada ya ajira ukawa unaikuza biashara hii na ikakuletea mafanikio makubwa sana.
Inawezekana wewe hujawahi kufikiria kua tajiri au kumiliki mali nyingi biashara zako na kadhalika lakini kujiajiri au kuwa na kipato cha ziada ni kitu cha muhimu kwa maana unakua hutegemei mshahara peke yake. Lolote linaweza kutokea kipindi hiki.
Kuwa makini na jitengenezee njia za kujisaidia kabla mabaya hayajakufikia.
Tafakari, Chukua hatua
Huku ukimtanguliza Mwenyezi Mungu mbele📖
Subscribe to:
Posts (Atom)