Sunday, June 4, 2017

VITU GANI VINAVYOFANYA NDOTO ZA MTU ZISIFANIKIWE

Kuna vitu vingi vinavyofanya mtu asifikie kile alichokuwa anategemea kukifanya kwa siku za usoni. Hizi ni baadhi ya sababu za kwa nini ndoto hazifnikiwi
  1. Kumwambia kila mtu ndoto yako: kwa upande mmoja ni sahihi kabisa  kumwambia mtu ndoto zako ambaye unadhani ataweza kukusaidia kufikia hiyo ndoto yako na siyo kumwambia kila mtu ndoto zako kwani wengine watakukatisha tamaa. Mfano unataka kufanya jambo fulani kwa siku za hapo baadae alafu unamshirikisha ndoto zako mtu ambaye huwa ana mawazo/mtazamo  hasi au tofauti kwa hicho ulichomweleza, 
  2. Kurithika: adui mkubwa wa mafaniko yako ya sasa ni mafanikio yako ya zamani. Watu wengi wamekuwa wakijikuta hawafikii zile ndoto zao kwa sababu ya mafaniki madogo waliyoyapata wakati wakiwa njiani kufikia zile ndoto zao. Kiabaya zaidi kwenye kurithika ni kwamba inafanya mtu siyo tu kushindwa kufikia ndoto zake bali pia kusahau ndoto zake. Mfano kwa mcheza soka ana ndotoza kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania lakini akishafika simba au Yanga anaridhika na kuhisi amefikia mafanikio makubwa sana. Tumia mfano huu uweke kwenye maisha yako ya kawaida. 
  3. kushindwa mara kwa mara: hapa kuna na mtihani mkubwa kwa watu wengi kuvuka kwani imeshakuwa desturi watu kuangali kitu kilicho washinda watu wengine na kuona kama na wenyewe kita washinda. Mfano utasika mtu anasema "kitu fulani kilimshinda mtu fulani, mimi ndiye nitakaye kiweza?" ukiangalia maneno kama hayo yanaonesha kuwa watu wengi wanaangalia watu walioshindwa kwa kufanya kitu fulani lakini wanasahau kuwaangalia watu waliofnikiwa kwa kufanya kitu cha aina hiyo hiyo moja. 
  4. kokosa ujasiri/udhubutu/kujiamini; hivi ni vitu tofauti ila kwa hapa vinaweza vikawa vinaleta matokeo ambaye yanaweza kuwa yanafanana. kuto kujiamini husababishwa na tabia kwani kwa zaidi ya 80%  ya vitu tunavyofanya vinatokana na tabia.  Kwa hiyo mtu akiwa hajiamini/adhubutu/ajaribu vya kutosha inakuwa ni vigumu kwa yeye kufikia ndoto zake. Mfano mtu anataka kuanzisha biashara ila anaogopa kufungua/kufanya hiyo biashara kwa hofu tu atapata hasara 
HAYO NI  BAADHI YA MACHACHE YA KUZINGATIA ILI NDOTO ZAKO ZISIFE AU ZISIISHIE NJIANI.

No comments:

Post a Comment