Showing posts with label HABARI. Show all posts
Showing posts with label HABARI. Show all posts

Tuesday, May 30, 2017

ANGELA KAIRUKI: HAKUNA AJIRA ZA WALIMU WA SANAA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, (Angela Kairuki) amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za sekondari

Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kusisitiza kwamba  kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao 
"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya" -alisema Angela Kairuki 
Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017 watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.

"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721 wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi 52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma"  -alisema Kairuki

KAIRUKI

Angela Kairuki: Walimu wa sanaa hawataajiriwa

kairuki

Tuesday, April 18, 2017

MAELEZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI.

1. Malimbikizo ya salary, yatalipwa automatic baada ya areas kuwa approved na maafisa utumishi, kuanzia pale ulipopanda. Hakuna tena kudai area

2. Uhamisho, kuhamisha mshahara ni jukumu la mwajiri wa awali, kama umehama

3. Kuhama mkoa ni lazima jina litokee kwenye orodha ya watumishi wanaohama.

4. Kwa wastaafu wanaodai areas, wanatakiwa kujaza fomu na viambatanishi ili ulipwe.

 5.Malimbikizo ya mshahara kuonekana kisha kufutika, haijapotea ila inahitaji kuidhinishwa upya.

6.Kama hujapata areas, na madai ni ya muda mrefu fuatilia kwa afisa utumishi ili ujaze form maalum.
7. Ukipanda cheo, kiri haraka.

8.Posho za safari za kikazi zinatokana na status ya mtumishi,  upandishaji wa vyeo vya watumishi hutegemea vikao vya DED, upandaji cheo inategemea fungu lililopangwa, mtumishi haruhusiwi kudai cheo. Hii ni kanuni. Promotion ni motisha kwa watumishi, si automatic. Mwajiri lzm apate taarifa za utendajikazi wa utumishi ndipo aandae promotion.

9.Madai kwa watumishi waliohama, yatashughulikiwa na mwajiri wa sasa baada ya kuwasiliana na mwajiri wa awali.

10. Upatikaji wa nyaraka, www.utumishi.go.tz na www.tamisemi.go.tz  utapata nyaraka na huduma kwa kutumia simu au computer.

11. Nauli za likizo, inategemea bajeti ya halmashauri, ilipwe kabla ya kusafiri, akijisafirisha atadai. Maombi ya nauli za likizo yatahakikiwa kwa kutumia nauli za SUMATRA. Marufuku kulipwa nusu nauli.

12. Kusoma nje ya nchi, kama upo kwenye mpango wa mwajiri utalipiwa na kulipwa mshahara, kama haupo mwenye mpango, utachukua  likizo bila malipo. Kibali kitatolewa na katibu mkuu kusafiri nje.

13. Rufaa ya matibabu, mwajiri alipe nauli na posho ya kujikimu. Ukijigharamia, mwajiri anatakiwa kukulipa.

14. Kutofautiana kwa mishahara kwa watumishi wenye sifa zinazofanana, kuna tume ya job evaluation inafanya utafiti hatua za mwisho, pia tatizo lilikuwa tsd kutoshirikiana na mkurugenzi.  Lkn tsd imekuwa tsc, tatizo litakwisha.

15. Disturbance allowance italipwa kwa 10% ya mshahara wake wa mwaka. Kwa watumishi waliohama destination, hata kama ni ndani ya km5.

16. Kumbuka kutunza nyaraka, kufuatilia mifuko ya jamii na michango ili kuhakiki uwasilishaji wa michango kabla ya kustaafu

17.Uteuzi wa wakuu wa idara huzingatia: utendaji kazi, uongozi, royality, elimu, nk.

18. Tange kwa kila kada ijazwe na kuwasilishwa kwa afisa utumishi.

19. Waliocheleweshwa kupanda daraja, wanatakiwa kwenda kwa afisa utumishi ili ajenge hoja ya kupanda kwa mseleleko na kuomba kibali kwa katibu mkuu.

20. Kama uliwekwa kwenye mpango wa mafunzo halafu ukajilipia, mwajiri anatakiwa akurudishie gharama alizotakiwa kukulipia.

21. Punguzo la kodi ya mshahara 9% linahusu wenye mishahara ya chini. Mfano katibu mkuu anakatwa 30% ya mshahara.

22.May 2016 promotion zilisitishwa pamoja na mishahara ilisitishwa kwa ajili ya watumishi hewa. Vyeo vyao vipo, ila marekebisho yao yamesitishwa. Watarejeshwa ktk vyeo vyao vipya muda si mrefu

23. Uhakiki bado serikali kuu.

24.Vyeo vya kielimu ktk nchi kimuundo ni mpaka 1st degree.  Masters, phd ni sifa za ziada tu.

25. Mishahara ya watumishi italingana na uzito wa kazi, miundo ya utumishi kurekebishwa ili watu wasifike bar/vidato vya mshahara.

26. Madeni yaliyokataliwa, yafuatiliwe ili kama ni tatizo la document, zitafutwe na kuprossess upya deni.

27. Walimu wa sayansi wanaofundisha na kufanya laboratory technicians wapewe allowances. Wataalam wa laboratory wanaandaliwa.

28. Kukaimu madaraka mwisho miezi 6, athibitishwe au asitishwe.

Monday, April 17, 2017

VIASHIRIA VYA VITA YA TATU YA DUNIA

Kumekuwa na wasi wasi wakuibuka kwa vita ya tatu ya dunia, katika vita hivyo vinavyodhaniwa itaweza kutokea baada ya mgogoro kati ya Marekani na Korea Kaskazini juu ya majaribio ya silaha za nyukilia yanayo fanywa na Korea Kaskazini
Hali hii ilifikia hapa baada ya Marekani kuelekeza meli yake ya kivita kutokea bahari ya Pacific  na kuchagizwa zaidi na maneno ya raisi wa Marekani Donald Trump ambapo alioneshwa kuchoshwa na kutoendelea kuivumilia Korea Kaskazini kwa majaribio ya nyukilia 
Raisi wa Korea Kaskazini baada ya kuona kitendo cha Marekani kuonesha nia ya kuingilia Korea kivita, amesema hata nyamaza bali ataishambulia Marekani kwa sila zake za nyukilia 
 
China imezishauri nchi zote mbili kuwa hakuna mshindi katika vita. China inajaribu kukaa kando isi jiingize katika vita hii japo kuwa inaoneka kuwa ni vita baridi.  
 
Thursday, April 13, 2017

MH. MAKONDA ATEMBELEA UJENZI WA HOSPITALI CHANIKA

Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Kinamama ya Chanika unaofadhiliwa na ubalozi wa Korea Kusini na kugharimu zaidi ya Tshs. 8.8 Bilioni uliokamilika kwa 90% hadi hivi sasa.
Mwanzoni 2016 Mh Makonda alipeleka maombi (propasal) ya kuomba washikadau wa maendeleo mbalimbali ikiwemo ubalozi wa Korea Kusini kusaidia katika ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mama na Mtoto , ambapo ubalozi huo ulikubali propasal hiyo
Ujenzi wa hospitali hiyo unaenda sambamba na ujenzi wa nyumba 28 ajili ya wauguzi na madaktari watakaohudumu hospitali hiyo masaa 24. Mpaka sasa 90% ya ujenzi huo imekamilika na kazi ya kufunga vitanda 160 vya wagonjwa na 10 vya kujifungulia na ufungaji wa vifaa vingine inaendelea kwa sasa.
Hospitali hii itakuwa ni mahususi kwa wakina mama na Watoto inatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh Magufuli