Saturday, December 10, 2016

FAHAMU MAGARI MATANO YANATUMIA MAFUTA KIDOGO INAKUFA KUENDESHA TANZANIA :


Kwa miji kama Dar es salaam na Arusha kukaa kwenye foleni mdaa mrefu haipotezi muda tu pia matumizi ya mafuta yanakua makubwa. Japo kuwa unaweza kupunguza matumizi ya mafuta kwa kuzima AC na kuendesha gari kwa mwendo/speed ya wastani lakini ukiwa na gari lenye kutumia mafuta kidogo unaweza kuokoa gharama zaidi na gari lenye kuuzwa chini ya milioni 15. kwa hiyo kama unafikiria kubadili gari lako au kununua gari lakom la kwanza basi ya ndio baadhi ya magari unaweza nunua yatumiayo mafuta kidogo:

1. toyota IST:
nathani utakuwa kipofu kama hujui kama toyota ndio inaongoza kwa kuwa na wateja wengi hapa nchini kwa mujibu wa best selling cars gari moja(1) kati ya manne(4) ni la toyota model. Na kwa sasa Toyota IST ndio maarufu zaidi. Bei ya Toyota IST inategemeana na mwaka iliyo tengenezwa na bei huwa kati ya milioni 8 hadi milioni 12.
Image result for toyota ist

2. Toyota Vitz:
hili gari halina tofauti sana na IST katika utndaji wake wakazi lakini hili lina umbo dogo zaidi na bei yake ipo chini zaidi ukilinganisha na IST na kwa udogo wake unaipa injini kuwa na nguvu zaidi na kutumia mafuta kidogo. Hili pia bei yake inategemea na mwaka lililo tengenezwa.
Bei yake ni kati ya ml 6 hadi 9
 Image result for toyota vitz used

3. Toyota Passo:
katika muundo na ufanyaji kazi wake hauna tofauti sana na Vitz lakini Passo ina umbo kubwa zaidi na ina uwezo wa kubeba watu watano huku ikiwa imebeba mizigo na huenda 33.5 mpg au 7 L/ 100 km. Unaweza kutumia 40,000/= kwa wiki kwenda umbali wa km 35 mpaka 40.
Bei yake huwa kati ya ml 6 hadi ml 8.5
 Image result for toyota passo used

4. Nissan March:
Sasa tunakutana na model ambayo siyo ya toyota. Japo kuwa ni kidogo sana kina okoa gharama nyingi za mafuta kinapendwa na madereva wa Tanzania kwa sababu kinauwezo wa kupenya kwenya foleni katika ile midaa ya haraka.
Bei yake huwa kati ya ml 2.5 hadi .5 kutegemeana na mwaka iloyo tengenezwa na umbali iliyotembea
 Image result for 2002 nissan march


5. Honda Fit:
model nyingine isiyokuwa ya toyota nayotumia mafuta kidogo . Inauwezo wa kwenda mpaka 33 mpg au 7.1L/100 km. Bei yake pia inategemeana na mwaka wa kutengenezwa na bei yake huwa kati ya ml 8 mpaka 14
 Image result for Honda Fit
Email:  godwinmasanja675@gmil.com

Phone: 0675333715

Whatsapp: 0683726851