Pamoja na yote hayo, hapa naomba niseme jambo moja. Sitaki kusema shindano hili ni halali/legit kwa 100% lakini nilichofanya kabla ya kuleta mada hii ni kuichambua kampuni inayoendesha shindano husika. Assumption ni kwamba, ikiwa shindano husika linaendeshwa na kampuni halali basi HUENDA na shindano lenyewe likawa halali. Nilichofanya mimi ni kutumia taarifa zilizotolewa na kampuni husika kisha nikazichunguza kwa kupitia external sources.
Ikiwa utahitaji kulisoma kwa makini shindano lenyewe na ikiwa unataka kujaribu, basi linapatikana hapa https://carfromjapan.com/en/campaign/car-from-japan-grand-giveaway-2017?refer=58bcf7b88abb210001e449d2
UTAFITI WANGU & SUPPORTING EVIDENCE
1. Physical Address: Kwanza nilichukua physical address iliyowekwa na hiyo kampuni. Adress yao ni hii hapa chini:
Nikataka kufahamu ikiwa kweli hiyo address ipo na hiyo kampuni inapatiakana kwenye hilo jengo. Google Map na Google Street Map ikathibitisha hayo yote mawili:
EVIDENCE 2: Japan Used Motor Vehicle Exporters Association (JUMVEA):
JUMVEA ni Jumuiya ya Wasafirishaji Magari huko Japan na wamethibitishwa na Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan. Watu wanashauriwa kabla ya kuagiza gari/magari kutoka Japan wahakikishie kwanza kampuni wanayotaka kufanya nayo biashara ni mwanachama wa JUMVEA.
Ukitaka kuufahamu UHALALI wa JUMVEA soma angalizo la Ubalozi wa Kenya nchini Japan. Screenshot na link ya habari husika ni hii hapa.
Kwahiyo hapo utaona Ubalozi wa Kenya unawaasa Wakenya kabla hawajaagiza magari wahakikishe dealer husika ana uhalali wa kufanya kibiashara na amesajiriwa na JUMVEA. Bila shaka ushauri huu ni muhimu hata kwetu sisi Watanzania. Aidha ni ushauri mzuri kwako hata kama huna haja na hili shindano.
Hapa nikataka kujiridhisha ikiwa kampuni inayooendesha hili shindano imesajiriwa na JUMVEA na nimethibitisha ni kampuni halali inayofanya biashara halali na ni mwanachama wa JUMVE. Hata hivyo, unaweza kuthibitisha wewe mwenyewe mbali ni hizi screenshots:
Ikiwa hadi hapo umeridhika na ungetamani kujaribu bahati yako, hilo linafayika kwa kutumia hii link: Free Car Giveaway
Kama vipi, tuendelee na uchambuzi wetu. Ukiangalia kwenye hiyo screenshot, unakuta hao Car From Japan ni Safe Trade Member. Safe Trade Member ni Car Exporter anayekuhakikishia usalama wa pesa yako wewe mnunuaji hata kama pesa umeshamtuma lakini gari haijasafirishwa. Bila shaka, kampuni inayoingia kwenye hili group ni lazima ithibitishwe ina uwezo wa kufanya biashara bila magumashi:
Kwa mara nyingine, hata kama huna haja ya kujaribu hili shindano kumbe tayari na wewe utakuwa umefaidika na taarifa hiyo hapo juu siku utakapotaka utakapotaka kuagiza gari kutoka Japan. Ili kujihakikishia usalama wa pesa yako, hakikisha dealer husika ni member wa Jumvea Safe Trade. Kwa maelezo zaidi, hawa ndio JUMVEA
Kwa hofu ya kuifanya makala hii kuwa ndefu sana, naomba niishie hapa lakini sina shaka wengi wetu tutakuwa tumejiridhisha kwamba shindano husika linaendeshwa na kampuni halali inayofanya biashara kihalali na inatambuliwa na mamlaka husika. Kwahiyo, ikiwa unataka kujaribu bahati yako, unaweza kufanya hivyo kupitia link: Free Car Giveaway
hii imechukuliwa
JF By
No comments:
Post a Comment