Saturday, April 15, 2017

UFAFANUZI JUU YA MAJINA MATATU YALIONEKANA KWENYE ORODHA YA AJIRA ZA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI

Baada ya TAMISEMI kutangaza ajira za walimu wa sayansi na hesabu, kumekuwa na maswali mengi watu wakijiuliza kuhusiana na majina yaliyo onekana wenye orodha hiyo kwani walimu wa masomo waliyopangwa sio wa masomo ya sayansi wala hisabati. katika orodha hiyo kuna walimu ambao wanafundisha masomo haya history & Geography, Book Keeping &Commerce na history & kiswahili ambayo yote siyo masamo ya sayansi wala hisabati.
Maswali watu waliyokuwa wakijiuliza ni pamoja na: ni kwa nini serekali inasema walimu wa sanaa wamezidi lakini bado wana ajiri wengine je huu sio upendeleo?, Je ni kilichowafanya hawa watu watatu nao wakaomba kuajirwa kwani walio ajiriwa waliomba kwa kutuma vyeti vyao? Je wakati wanapanga haya majina hawakujua majina matatu siyo ya sayansi?

Kutoka na habari nilizozipata mambo yapo hivi: hayo majina matatu ni majina ya walimu ambo walikua wanafundisha shule ambayo ilikua inamilikiwa na CCM kabla haijachukuliwa na serikali kwani Raisi alaichukua hiyo shule na kuifanya mali ya serekali kwa hiyo majina ya walimu hao yameongezwa ili kuwanya wawe wajiriwa rasmi wa serikali

No comments:

Post a Comment