Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Kinamama
ya Chanika unaofadhiliwa na ubalozi wa Korea Kusini na kugharimu zaidi
ya Tshs. 8.8 Bilioni uliokamilika kwa 90% hadi hivi sasa.
Mwanzoni 2016 Mh Makonda alipeleka maombi (propasal) ya kuomba
washikadau wa maendeleo mbalimbali ikiwemo ubalozi wa Korea Kusini
kusaidia katika ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mama na Mtoto , ambapo
ubalozi huo ulikubali propasal hiyo
Ujenzi wa hospitali hiyo unaenda sambamba
na ujenzi wa nyumba 28 ajili ya wauguzi na madaktari watakaohudumu
hospitali hiyo masaa 24. Mpaka sasa 90% ya ujenzi huo imekamilika na
kazi ya kufunga vitanda 160 vya wagonjwa na 10 vya kujifungulia na
ufungaji wa vifaa vingine inaendelea kwa sasa.
Hospitali hii itakuwa ni mahususi kwa wakina mama na Watoto
inatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh Magufuli
No comments:
Post a Comment